Vertalingen

De gebedsnoot in het Swahili

Swahili

Mbegu ya sala.

Kwenye Rijksmuseum Amsterdam mtu moja amenionyesha kitu fulani toka kwa wakati baina ya A.D. 1000 - A.D. 1600, kitu hicho ni mviringo kimetengenezwa toka kwenye mbao ya mti wa mnazi. Mviringo huo umegawanywa nusunusu waliutengeneza kwa uangalifu sana. Kwenye mviringo inaonyesha picha au sanaa, kama mfano wa kuzaliwa na msalaba wa Yesu Kristu. Zile mviringo waliweka bawaba na unaweza kufunga kama kabati. Kitu hicho ilikuwepo ndani ya mviringo wa shaba. Na mviringo wa shaba ulikuwepo ndani ya mfuko wa ngozi ya wanyama. Injili inakuwepo ndani ya mviringo huo. Kitu hicho imetengenezwa kwa ajili ya kuchukua safarini. Baada ya miaka michache nimekuwa na mawazo kutumia, "mbegu hii ya kusali" kwa namna nyingine. Lli watu waitumie tena. Sasa hivi mviringo huo umetengenezwa kama haina ya bapa na unaweza kuandika ndani ya kitu hicho kwa mfano, sala, tarehe, n.k. kama kumbukumbu. Hii mbegu ya kusali ni rahisi kwa kuhifadhi au kutunza. Hivyo unaweza kuchukua "mbegu ya sala" hii kila mahali popote unapokwenda. Wakati unataka kubadilisha unaweza kuvuta kwa kuzugua kwa msasa na kuandika kitu kingine.